Mwenyekiti wa CCM aliemaliza mda
wake Othman Gora ametetea kiti chake baada ya kuwabwaga wagombea wenzake
kwa kura 676 sawa na asililimia 76 ya kura zote 1092 zilizopigwa katika
uchaguzi ambao siku mbili kabla ya uchaguzi huo viongozi walionekana
wakitoa rushwa za wazi kwa wajumbe ilikujipanga na uchaguzi mkuu 2020
Makundi ya uchaguzi huo ambao
wajumbe walianza minong’ono kabla msimamizi wa uchaguzi huo hajatangaza
matokeo, wapambe walianza kumtangaza mgombea Gora kuwa ameshinda bila
kujali kanuni za uchaguzi ambapo hapo kabla ya kufika ukumbini wajumbe
walionekana wakikaa vikundi na kupewa fedha kiasi cha Elfu kumi na
kupewa maelekezo ya nani anaetakiwa.
Wajumbe 1092 zaidi ya asilimia
98.99 ambao walishiriki kupiga kura, ambapo wagombea kwa nafasi mbali
mbali walikuwa nafasi ya mwenyekiti wakiwa 3 nafasi ya ujumbe wa mkutano
mkuu taifa wakiwa 9 na wajumbe halmashauri kuu wilaya wakiwa 6 na
wajumbe nafasi ya uwt wilaya 7 nafasi ya wajumbe kutoka kundi la vijana
wakiwa 7.
Akisoma matokeo hayo majira ya saa
7.15 usiku Msimamizi wa uchaguzi huo Mbunge wa Mtera na mjumbe wa
halmashauri kuu taifa Job Lusinde alimtangaza Othman Gora kuwa mshindi
wa kiti cha uwenyekiti wa wilaya hiyo kwa kuwabwa wenzake Kimolo Iddy na
Juma Fataki.
Lusinde alisema kuwa uchaguzi huo
ambao ulienda kwa uwazi na kuwapata viongozi hao ambao wataongoza kwa
kipindi cha miaka mitano na kuwataka wale ambao kura hazikutosha
wajipange kwa uchaguzi ujao na kuwa kitu kimoja katika kukijenga chama
hicho.
Akizungumza mara baada ya
kutangazwa Othman Gora alisema kuwa ushindi aliopata ni wanaccm wote na
kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha chama hicho kinaendelea
kuimarika na kushinda chaguzi mbali mbali ikiwemo kuibua miradi ya
maendeleo na kuisimamia serikali.
Kwa upande mwingine wajumbe
wameulalamikia uchaguzi huo uliogubikwa na matukio ya rushwa za wazi
wazi zikiongwa na naibu waziri wa fedha dakta.Ashatu Kijaji kwa upangaji
wa safu yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hali iliyopelekea
wajumbe kupewa fedha wakitumia Makati wa ccm wa Kata na baadhi ya
madiwani.
Hata hivyo baadhi ya wagombea
wamekuwa wakiendelea na vikao vya chini kwa chini lengo likiwa ni kukata
rufaa kwani uchaguzi huo kanuni na sheria zilikiukwa kwa kutangaza
matokeo kabla ya msimamizi hajatangaza hali katika mkutano huo ambao
uliendeshwa kwa uwazi lakini ukiwa na kasoro za upangaji wa matoke.
Pamoja na kuwepo taasisi ya
kupambana na rushwa TAKUKURU na kupewa taarifa za wazi bado hatua
hazikuchukuliwa kwa wakati lakini mwanahabari hii juzi usiku katika kata
ya Soera alishuhudia wajumbe wakipewa fedha na bwana aliefahamika kwa
jina moja Ridhiwan.
Aidha pia huko kwenye kata za
Bumbuta,Kisese,Kikore wajumbe walipewa mlungula wa wazi ambapo Naibu
waziri alidai ametumwa na makamu wa Rais na mwenyekiti wa vijana kata ya
Bumbuta Hemed alitishiwa kutolewa dirishani kwani ameonekana kumpinga
Dkta Kijaji katika malengo yake
No comments:
Post a Comment