• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 31 October 2017

    RC Makonda kufufua magari 10 ya vyombo vya usalama





    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewapiga marufuku wanasiasa ambao wanaeneza maneno ya uchochezi katika mkoa wake na kuwataka wananchi wawapuuze.
    RC Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa anakabidhi magari 10 kwa kampuni ya DAR COACH kwa ajili ya matengenezo ambayo yatakamilika kwa muda wa siku 110 huku gharama yake ikiwa ni zaidi ya bilioni 1.
    RC Makonda ameeleza kuwa wanasiasa wa namna hiyo hawahitaji katika Mkoa wake, vinginevyo ni vyema washirikiane kuijenga Dar es Salaam mpya.

    " Kauli za kebehi, kutukanisha, kufarakanisha na kuchonganisha hazitusaidii katika ujenzi wa Dar es Salaam mpya, hivyo ni waombe na ninafikiri wanafahamu mimi siyo muoga na katika watu wanaojiamini katika Mkoa huu ni mimi hapa, kwenye nchi atabaki Rais, na katika wakuu wa Mikoa wanao jiamini mimi najitosha, nisinge penda tujaribiana na kuchafuliana miji, kama unataka kutoka kauli ya uchochezi katolee kwenye Mkoa wako, na nimepata taarifa mmoja mnae kaeni nae ". Alisema RC Makonda.


    RC Makonda ameshangaa kuona wanaosema serikali imepoteza dira huku akisema serikali ya awamu ya tano imefanya makubwa ikiwemo suala la Rais kuidhinisha fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, elimu bure kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, kulipwa kwa deni la zaidi ya trilioni 1 ambalo serilai ilikuwa inadaiwa na taasisi mbalimbali.
    Unasema dira hakuna wakati wanafunzi walikuwa wanalipa ada, wakati huu hawalipi, unasemahuoni dira wakati wanafunzi walikuwa wanagoma kwa kukosa mikopo Rais anaidhinisha unasema huoni dira, nchi ilikuwa haina ndege serikali imeleta ndege unasema huoni dira, reli ya starndard gauge inajengwa gharama za serkali unasema huoni dira, kweli kuna haja ya kuwa na hospitali ya milembe kwenye kila mkoa" Alisema RC Makonda.
    Siku ya jana aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, alijiuzulu nafasi yake ya Ubunge wa Singida Kaskazini na nyadhiza zake zote za ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai serikali ya awamu ya tano imepoteza dira jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda analipiga marufuku.
    Vilevile siku ya leo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutoa maneno ya uchochezi katika ufunguzi wa kampeni za udiwani kata ya Kijichi wilaya ya Temeke, jambo ambalo Mkuu wa  Mkoa amepiga marufuku kwa mwanasiasa yeyote kufanya uchochezi badala ya kuhamasisha maendeleo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI