Waziri wa Biashara,viwanda na
masoko Balozi Amina Salum Ali amesema vikwazo vya kibiashra baina ya
Zanzibar na Tazania bara inaendelea kufanya mazungumzo na watendaji wa
taasisi za Tanzania bara ili kuondosha vikwazo vya kibiashara baina ya
pande hizo mbili.
Hayo ameyasema leo huko baraza la
wakilishi chukwani katika kikao kinacho endelea barazani hapo wakati
akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la paje Jaku Hashim Ayuob alietaka
kujuwa kwanini hivi karibuni serikali ya jamuhuri ya mungano wa
Tanazinaia ilifanya mazungumzo na Serikali ya Kenya kutatua changamoto
za kibiashara baina ya nchi hizo na mazungumzo yao yamekuwa ya mafanikio
makubwa kwa kupitisha didhaa baina ya Kenya na Tanzania zimetatuliwa .
Je,kwanini kwa upande wa Zanzibar
na Tanzania bara kwa mda mrefu kumekuwa na changamoto za wafanya
biashara wa Zanzibar kufanya biashara bila ya Bughudha Tanzania bara
licha ya jambo hilo kuwa la muda mrefu bado changamoto hizo zipo kwa
miaka mingi zikiwa nchi zao zina udugu wa damu kwa mda mrefu.
Waziri alisema vikwazo vya
kibiashara baina ya Kenya na Tanazania ,Kenya iliwekea vikwazo Tanazania
katika bidhaa ya unga na bidhaa ya gesi na hivyo kusababisha usumbufu
wa biashara kwa upande wa Tanzania.
Alisema na kwa upande wa Tanzania
nayo iliwaekea vikwazo Kenya katika bidhaa za maziwa na sigara kuingia
ndani ya soko la Tanzania nayo ikawaekea vikwazo yasiingie Tanzania
,baada ya jambo hilo kupelekwa ngazi za juu viongozi wakuu wanchi hizo
mbili wamekubaliana kuondolewa vikwazo baina ya nchi zao mbili ,na
makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano uliofanyika septemba 8, 2017
mwaka huu.
Alisema kwa upande wa vikwazo vya
kibiashara baina Tanzania Bara na Zanzibar wizara yake inaendelea
kufanya mazungumzo na watendaji wa taasisi za bara ili kuondosha
vikwazo baina ya nchi hizo mbili.
Waziri huyo amesema hivi
karibuni wizara yake ilikuwa na kikao na wizara ya viwanda ili kuangalia
matatizo yanayo wakabili wafanya biashara wanchi zao mbili.
Aidha waziri huyo alisema kuwa
kupitia kamati ya kusimamia masuala ya vikwazo vya kibiashara visivyo
kuwa vya kiushuru kamati hiyo imeundwa ili kufuatilia changamoto hizo
ili hatimaye kuendelea kuzitatuwa na kuzipatia ufumbuzi muafaka.
Hata hivyo waziri huyo alisema
suala la vikwazo vya kibiashara baina yao litazungumzwa kwenye vikao vya
mashirikiano baina SMT na SMZ vinavyo fuata.
No comments:
Post a Comment