Wafuasi wa muungano wa upinzani
nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) wamejitokeza katika baadhi
ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa kazini kwa baadhi ya maafisa
wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.Muungano wa Nasa ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Hayo yakijiri, mabalozi kutoka nchi kadha za Magharibi wameilaumu serikali ya Kenya pamoja na upinzani, kabla ya kufanyika kwa shughuli za upigaji kura baadaye mwezi huu.
Kwa njia ya taarifa ya pamoja wanadiplomasia wa mataifa 13 na jumuia ya bara Ulaya EU, walikosoa upinzani nchini Kenya kwa kutishia kususia marudio ya uchaguzi mkuu, na chama tawala kwa kujaribu kubadilisha sheria za uchaguzi katiba kabla ya marudio ya uchaguzi huo mkuu.


Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti
mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika
uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment