Chama cha mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika kata 42 kati ya 43
zilizofanya uchaguzi mdogo wa udiwani jumapili ya Novemba 26 kwenye
mikoa 19 nchini.
Polepole amesema kuwa Chama chake kimeibuka na ushindi huo katika kata hizo ikiwa ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya CCM.
Polepole ameitaja kata ambayo chama chake kimekosa ushindi kuwa ni Ibigi iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambayo imechukuliwa na mgombea wa CHADEMA. Aidha Polepole amedai kuwa chama kimeumia kwa kuikosa kata hiyo lakini kimekubali matokeo.
Kwa upande mwingine Polepole amezitaka mamlaka kushughulikia haraka baadhi ya dosari zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo, ambayo chama hicho kimeripoti kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi ikiwemo vitendo vya vurugu vilivyofanywa na watu wasiokuwa na nia njema
No comments:
Post a Comment