Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kununua kondomu
zitakazosambazwa nchi nzima bure, kwa lengo la kupunguza maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi.
Akiendelea kuelezea suala hilo Dk. Rusibamaila amesema kutakuwa na mashine maalumu zitakazofungwa kwenye maeneo ya sehemu za starehe kama baa, nyumba za kulala wageni, migodini na katika kumbi za burudani, lakini takwomu zinaonyesha licha ya kuwa na ufahamu wa faida ya condom, idadi ya wanaoutumia ni chache zaidi.
“Takwimu zinaonyesha kwamba 69% ya wanawake na 77% ya wanaume wanafahamu kwamba kondomu inaweza kuzuia VVU, lakini ni 27% tu ya watu wenye wenza zaidi ya mmoja walitumia kondomu walipofanya ngono mara ya mwisho,” amesema.
Mkurugenzi huyo amesema kondomu hizo zitanunuliwa kupitia fedha za Global Fund, ili kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030
No comments:
Post a Comment