• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 27 November 2017

    Waziri Mwakyembe atembelea uwanja

    Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe leo ametembelea uwanja wa kumbukumbu ya  Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
    Waziri Mwakyembe akiwa ameambatana na Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na Kaimu Katibu mkuu wa TFF Kidao Wilfred amejionea maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
    Uwanja huo upo kwenye marekebisho ili kuboresha eneo la kuchezea (Picha) pamoja na majukwaa na maeneo mengine ya uwanja kama ubora wa vyoo na mabafu.

    Waziri Mwakyembe na viongozi hao wa TFF wameambatana na wenyeji wao ambao ni viongozi wa chama cha soka mkoani humo ARFA na wamewaonesha maeneo mbalimbali ya uwnaja huo ambayo tayari yameshaekebishwa na yake ambayo bado.
    Mwakyembe yupo mkoani Arusha tangu jana akiwa ameenda kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo ufunguzi wa ligi kuu soka ya wanawake Tanzania bara. Katika mchezo wa uzinduzi Allience Queens ya Mwanza ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI