Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani)
ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington kwa pamoja
wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam _Mh
Paul Makonda_ kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa huu kwa
kutoa makontena 36 ya samani mbalimbali zikiwemo viti vya kisasa
zaidi ya 5000,meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu
makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700.
Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za
kimarekani $ 800,000 ambazo ni sawa na shilingi 1,800,000,000 za
kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa
kupitia kampeni iliyoanzishwa na _Mh Paul Makonda_ mapema Agosti
mwaka huu.
Kupitia samani hizi adhma ya Mh Paul Makonda_ ya
kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa
Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya
kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kufikiwa kama matokeo ya
miundo mbinu rafiki kwa wote.
Makontena hayo yanatarajiwa kufika nchini mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mh Makonda_ amewashukuru wadau hawa ambao bila
kuzingatia umbali waliopo na nchi yao bado wameonyesha hari ya kuguswa
na changamoto za watanzania wenzao hapa nchini, na kutoa rai kwa
watanzania wengine kuendelea kuunga mkono kampeni hii ya ujenzi wa ofisi
402 za walimu Dar es salaam kwa namna watakavyo weza kwani hatma ya
ustawi wa maendeleo ya Tanzania ni wajibu wa kila mtanzania.
Imetolewa na kitengo cha habari na uhusiano,ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment