KAIMU Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema serikali imeweka mikakati maalum katika kuhakikisha wanawafichuwa waovu ikiwemo udhalilishaji.
Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja huko katika kiwanja cha Mpira Mkokotoni wakati akiendelea na ziara yake ya kiserikali akiwa ni kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili katika Wilaya zao.
Alisema hatua hiyo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwani vimekuwa vikiathiri jamii.
Alisema Mkoa huo ni mkoa ni miongoni mwa vitendo hivyo licha ya jitihada zinazochukuliwa na wanaharakati wa masulaya hayo ambayo mara nyingi wamekuwa wanavikemea na kuvipigia vita.
Hata hivyo aliliagiza Jeshi la Polisi Mkoa huo kulitilia mkazo sula hilo ikiwemo kulifuatilia tatizo lilojitokeza hivi karibuni kwa mtoto mwenye umri wa miaka mitano kufanyiwa kitendo cha kubakwa katika njia ya haja kubwa na ndogo kitendo ambacho hakiwezi kuvumiliwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa haraka.
Hivyo aliwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo ikiwemo kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria ili kuona vitendo hivyo vinaondoka kabisa katika mkoa huo.
“Hatupendi kuona kila wakati vitendo hivi vinatajwa midomoni tu sisi linatusikitisha kupita kiasi kwani tunashangazwa kwa nini mkoa huu tu hivyo jitihada tuzifanye ili tuweze kukomesha kabisa” alisema.
Mbali na hayo aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao katika kufuatilia nyendo zao kwa lengo la kunusuru jamii na janga hilo ambalo limekuwa linatishia kuharibu vijana ambao ni taifa la baadae.
Sambamba na hayo aliwataka wanaharakati kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuweza kupungua kwani vitendo hivyo vimekuwa vinakithiri sambamba kushirikiana na kufichua maovu ili serikali iweze kuviondoa kabisa.
Mbali na hayo aliwasisitiza wasimamizi wa sheria kulizingatia suala la dhamana kutoa kwa mujibu wa sheria na kwa kuangalia makosa yaliyokuwa hayatoleki dhamana wasizitoe ili wananchi kuwa na imani na vyombo hivyo.
“Huu utoaji wa dhamana uliofanyika kwa motto huyu tunawakatisha tamaa wananchi na kuwafanya kuwa wakose na imani ya vyombo hivi ila ni vyema kubadilika ili wananachi waweze kutoa mashirikiano ya kutosha kwani jamii imekuwa inatusema sana” alisema.
Sambamba na hayo alisisitiza kuwakamata wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili kuweza kuondosha kabisa suala hilo.
Akizungumzia dawa za kulevya Ayoub alisema ahakikisha wanafanya Operesheni maalum mkoani humo ya kukamata vikundi vyote vinvayojihussha na uuzaji na usambazaji wa dawa hizo pamoja na watumiaji wa dawa hizo kwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Hata hivyo alisema hatokuwa tayari kutoa suluhu kwa mtu yoyote atakayepatikana na kosa la kuuza ama utumia wa dawa za kulevya na atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment