• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 23 November 2017

    Madiwani Waikana Tarura

    MADIWANI wa Manispaa ya Ilala kwa Kauli moja wameilalamikia Mamlaka ya Barabara ya vijini na Mjini nchini (TARURA) kwa kushindwa kuzijenga na kuzikalabati Barabara  korofi zilipo ndani ya Manispaa hiyo.
    Akitbitisha Malalamiko hayo leo Jijini Dar es Salaam ,Naibu Meya wa Manispaa ya hiyo , Omari Kumbilamoto mara baada ya kumalika kikao cha Barala la Madiwani  wa Manispaa hiyo,
    Amesema katika kikoa hicho madiwani wametoa vilio vyao  kwa Tarura kwa kushindwa kujenga barabara hizo licha ya kupewa fedha na Halmashauri hiyo.
    "Madiwani wengi wamesitishwa na Tarura,wameona jinsi kwenye Kata zao barabara hazijajengwa na huku wengine wanasema hata zile mbovu hazijengwa,,na wanashangaa kwani sisi Halmashauri tulitenga zaidi ya Bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo lakini tunashangaa bado barabara ni mbovu"Amesema Kumbilamoto ambaye pia ni diwani wa Kata ya Vingunguti.
    Amesema kwa sasa  baada ya kutungwa sheria  ya uuzishaji wa Tarura Manispaa zimepokonywa jukumu la kusimia na kujenga Barabara jambo analodai limechangia kuwepo kwa Malamakiko kutoka kwa Wananchi kwa Madiwani.
    "Leo hii Tarura imeelemewa Barabara ni mbovu imeshindwa kuzisimamia,na wananchi wanatulahumu sisi wakijua sisi ndio kila kitu  ,lakini sheria imetupoka majukumu,"amesema Naibu Meya huyo ambaye ni Diwani wa Chama cha Wananchi (CUF)
    Hata Hivyo,Kumbilamoto ameishauri Serikali kuhakikisha wanaifuta Tarura ili kuweza kurudisha majukumu yanayofanywa na Tarura yaendelee kufanywa na Halmashauri ili malamiko hayo yapungue .
    Katika hatua nyingine wakati wa Kikao ,Manispaa hiyo imesema imejipanga kuhakikisha wanaboresha Afya za Wananchi wa Halmashauri hiyo kwa kutenga fedha kwenye Sekta ya Afya.
    Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victorina Ludovick amesema hayo wakati alipojibu akijibu swali la diwani wa Kata ya Mzinga, Isack Job.
    Diwani Job alitaka kufahamu mipango ya halmashauri katika kuboresha huduma za afya ili kupunguza idadi ya wanaojitokeza kwenye huduma za bure.

    Job ametoa mfano wa upimaji wa afya bure uliofanyika miezi michache iliyopita katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na unaoendelea sasa katika meli kutoka nchini China.

    Dk Ludovick amesema katika utafiti waliofanya imebainika watu wengi wanafuata huduma za bure za afya kwa kuwa wanashindwa kwenda kufanya vipimo  hospitalini kutokana na gharama kubwa.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI