• ..

    ..

    Thursday, 23 November 2017

    MAMC kuanza kazi rasmi jumamosi hii huku ikiwa imesheheni vifaa bora na vya kisasa zaidi.


    Na stahmil Mohammed
    Hospitali ya taaluma ya chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi muhimbili MUHAS iliyopo katika kampasi ya mloganzila, inatalajiwa kufunguliwa rasmi siku ya jumamosi tarehe 25 mwezi huu na mgeni rasmi atakuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, John pombe magufuli ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa mpaka hospitali hiyo kukamilika ambapo ujenzi ulikamilika rasmi mwezi agosti 2016.
    Akiongea Leo kaimu mkuu wa chuo Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema kuwa hospitali hiyo inatambulika kama MUHAS academic medical centre (MAMC) na imepewa hadhi ya hospitali ya Taifa ya rufaa yenye uwezo wa kutoa huduma za afya zinazohitaji madaktari bingwa na madaktari waliobobea.
    Pia amesema kuwa MAMC imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu na cha kisasa ili iweze kutumika katika kufundisha watalaam wa huduma za afya, kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa na kufanya tafiti za afya.
    Prof. kamuhabwa amesema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo umefanyika chini ya ufadhili wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mkopo laini (soft loan) kutoka serikali ya jamhuri ya korea.
    Aidha  Prof.kamuhabwa amebainisha matibabu yatakayokuwa yanatolewa hospitalini hapo na kusema kuwa hospitali ya taaluma na tiba ina vitanda vya kulaza wagonjwa 571, na ina vitengo vyote vinavyohitajika katika kutoa huduma za kibingwa ambapo ametaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni huduma za Tiba ya dharura na ajali kwa wakubwa na watoto, huduma za mfumo wa uzazi, huduma za upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za magonjwa ya akili huduma za magonjwa ya kinywa, huduma ya magonjwa ya mifupa na majeruhi pamoja na huduma za magonjwa wa macho, mfumo wa pua, koo na masikio.
    Profesa kamuhabwa amemaliza kwa kusema mradi huo umegharimu shilingi milioni94.5 dolla za kimarekani baada ya kupata mkopo laini kutoka korea ya kusini ambapo imetoa dolla milioni 49.5 za kimarekani na Tanzania imetoa dolla milioni 18.40.pia amesema  hospitali hiyo imekuwa na wauguzi wapya  na waliohamishwa mikoa249,wauguzi kutoka muhimbili 229,na imetoa vibali vya kazi 259 hivyo itakuwa na wauguzi zaidi ya 807 hivyo huduma zitafanywa kwa weledi

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI