Na stahmili Mohamed.
Ikiwa ni mwendelezo wa programu ya Museum Art Explosion inayofanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi iliyoandaliwa na Makumbusho ya Taifa ikiwa na lengo La kuwaleta wasanii na kutoa fursa ya kuonesha vipaji vyao na ufundi wa majukwaa na kuuza kazi zao kwa watanzania na wageni mbalimbali Makumbusho ya Taifa ikishirikiana na kundi La wasanii la Kaleleo sanaa Network wameandaa onesho la jukwaani la igizo LA "Fumo Liongo" ikiwa na lengo LA kurejesha hadhi na thaman ya majukwaa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa idara ya program Makumbusho ya
Taifa Bw.Chance Ezekiel alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na onesho hilo kuwa litafanyika hapo kesho saa moja kamili
usiku katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na mgeni rasmi atakuwa ni
Waziri wa habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
lengo ni kufufua Sanaa ambazo zinaonekana kupitwa kiteknologia.
Hata hivyo Bw .Azekiel amesema moja ya kazi za Makumbusho
ya Taifa ni kuhifadhi na kurithisha utamaduni wa mtanzania kwa vizazi
vilivyopo na vijavyo wameona IPO haja ya kurithisha utamaduni wa kazi
bora za sanaa za jukwaani kwa wasanii chipukizi na wapenda Sanaa kwa
ujumla pia tangu walipoanza program ya Museum Art Explosion kuna
faida nyingi zimepatikana ikiwa in kuinua hari za wasanii kwani hupata
fursa nyingi za mialiko nje ya nchi na Makumbusho hufaudika kwa
kuhifadhi kumbukumbu za kazi na historia za wasanii hao hususan
waluobibea katika tasnia hii.
Kwa upande wake msanii na muongozaji wa onyesho hilo Bw
Ghonche Materego amesema ni wakati wa kuthamini kazi za Sanaa za
majukwaa kwani zinamashiko zaidi pia amewataka wasanii ,wanafunzi wa
sekondari pamoja na vyuoni watanzania kiujumla kujitokeza kwa wingi
katika onyesho hilo ambalo linaonyesha na kuelezea historia ya MTU
maarufu na shujaa aitwae Liongo aliyeishi pwani ya Afrika Mashariki
katika karne ya 15 kwa shilingi elfu kumi tu kwa mkubwa na shilingi elfu
tano kwa mtoto zaidi ya yote watu wote watajifunza na kuburudika.
No comments:
Post a Comment