• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 28 November 2017

    Mashindano ya mchezo wa Baseball yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Azania kuanzia tarehe 30 November hadi Disemba 2017 jijini Dar es salaam.

    Na Stahmil Mohamed.
    Mashindano hayo yanatarajia kushirikisha timu 11 kutoka vilabu vya shule za sekondari za Iyunga kutoka mkoani Mbeya,Sanya juu kutoka Kilimanjaro,Songea Boys na Londoni kutoka Mkoani Ruvuma,Mchanganyiko wa sekondari kutoka mkoani Ruvuma mchanganyuko wa sekondari kutoka mkoani mwanza,Mwanakwerekwe C kutoka Zanzibar,Kibasila,Juhudi ya mkoani Dodoma pamoja na wenyeji Azania kutoka Mkoani Dar es salaam.
    Aidha kutakuwa kuwa na timu mbili za Tigers kutoka ilala na Giants ya Temeke ambazo zinaundwa na wachezaji ambao hawapo katika vilabu vya sekondari vilabu hivi vilianzishwa na wahitimu wa sekondari na ambao chama hakikutaka kuona vipaji vilivyoibuliwa vinapotea bila kulelewa katika mfumo ulio rasmi.
    Hata hivyo mashindano hayo yamepewa jina la5th Tanzania koshien National Baseball Championship yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Naibu waziri wa habari na utamaduni  mhe Juliana Shonza siku ya tarehe 1 Dec 2017 asubuhi.
    Vile vile wataalamu wa mchezo huo kutoja nchini japan wakishikiana na wataalamu wa hapa nchini kusimamia katika uamuzi na sehemu ya ufundi na baada ya mashindano hayo uteuzi wa timu ya taifa ya mchezo huo chini ya umri wa miaka 23 ambayo itashiriki mashindano ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika mkoani mwanza  na kushirikisha timu kutoka kenya,Uganda kuanzia tarehe 7 Disemba2017.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI