• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 28 November 2017

    Lema amjibu Mange Kimambi

    Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amemtoa wasiwasi mwanadada anayefahamika kama mwanaharakati wa mitandaoni Bi. Mange Kimambi kuwa asijali kwani wananchi watatoa maamuzi juu ya kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo Jumapili iliyopita.
    Lema amelazimika kumuondoa wasiwasi mwanadada huyo baada ya kuonyesha hisia za hasira kwaviongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakilalamika kufanyiwa madhamibi na Chama Cha Mapinduzi huku akiwataka wachukue maamuzi magumu.
    Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange amemwambia lema "Haki mnawachosha wananchi. Mpaka mnaonekana masnitch yani kama vile mnatumika na CCM. We need stronger leadership than this. Chukueni maamuzi magumu acheni kulia lia kama wajane..Mnafanya mpaka mtu unatamani kuwatukana"
    Baada ya Maoni marefu Mange aliyoyaandika, Lema amemjibub Mange kwa kumwambia;
    "Mange,nimekusoma/ nimekuelewa watu wana hasira kuhusu mambo yanoyoendelea nchini hususani ktk uchaguzi huu wa marudio ya udiwani,  kelele juu ya dhuluma hizi ni muhimu, acheni kwanza watu wote wajue kilio chetu, maamuzi ya dhati yatatoka kwa wananchi. Only Time will tell. Usiogope" Lema.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI