• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 28 November 2017

    Viongozi wakemewa na Waziri Jaffo

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Suleiman Jaffo, amesema, bila kusimamiwa kwa maadili katika jamii, taifa litashindwa kusonga mbele katika juhudi za kujenga jamii inayochukia rushwa.
    Akizindua Maadhimisho ya Maadili ya Kitaifa Mjini Dodoma leo, Mh. Jaffo amewakemea viongozi wote wanaokumbatia rushwa na kuziagiza mamlaka zinazosimamia maadili kuwachukulia hatua kali ili kupunguza tatizo hilo nchini.
    Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof. Mussa Assad, amesema, taasisi hiyo inaendelea kusimamia maadili na kupambana na rushwa pamoja na kusimamia maadili na haki za binadamu, hivyo kuendelea kuboresha ufanisi kwa jitihada za serikali.
    Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni wajibika piga vita rushwa zingatia maadili haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI