Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi imewasomea shitaka la mauaji watu
watatu wanaotuhumiwa kumuua kijana Humphrey Makundi aliyekuwa mwanafunzi
wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo
Moshi.
Upande wa Jamhuri katika shitaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah.
Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha wa pili Edward Shayo na wa tatu Laban Nabiswa, walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.
Aidha washitakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shitaka la mauaji huku akiwataka kusubiri kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.
Hakimu Mkazi Mawore, ameahairisha shitaka hadi Desemba 8 mwaka huu litakapotajwa tena na kwamba washitakiwa wote watarudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana
No comments:
Post a Comment