• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 28 November 2017

    WENGER ATOA JIBU KUHUSU OZIL,SANCHEZ KUONDOKA ARSENAL WAKATI WA DIRISHA DOGO

    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa mara nyingine amewazungumzia mastaa wake wawili, Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa kusema kuwa wataendelea kuichezea timu hiyo hadi mwisho wa msimu na kusisitiza kuwa hana mpango wa kuwauza Januari, mwakani.
    Kumekuwa na taarifa kuwa wachezaji hao wanaweza kuondoka kwa kuwa mikataba yao inaelekea ukingoni na hawajafikia makubaliano ya kusaini mikataba mipya, ili kuokoa fedha, ilielezwa kuwa Arsenal ingewauza karika usajili wa dirisha dogo la Januari, mwakani. 
    “Kichwani mwangu wataendelea kubaki hapa hadi mwisho wa msimu, labda kama kuna kitu cha ajabu kitatokea.
    “Kumekuwa na taarifa nyingi, je wataendelea kubaki hapa kwa muda mrefu? Hilo ni swali gumu kulijibu kwa sasa,” alisema Wenger.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI