Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amefafanua, “Katiba mpya inahitaji gharama kubwa na sisi tumeanza na kutatua changamoto za jamii kwanza, ikiwemo mahitaji ya maji, changamoto za elimu, na sekta ya Afya”. Amesema Waziri Mkuu
Waziri Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo.
“Kila bajeti ina vipaumbele vyake, kwa sasa acha tufanyie kazi vile ambavyo vinasumbua wananchi wengi kwani kipaumbele kikuu ni kuimarisha huduma za jamii hivyo tunasimamia ukusanyaji mapato ili tumalize changamoto hizi na katiba ni muongozo tuu acha tutumie huu uliopo sasa”. Amesema Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment