• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 9 November 2017

    Nassari amkalia kooni Bashe

    Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari  (CHADEMA) amemvaa Mbunge wa Nzega Mjini, Mh. Hussein Bashe (CCM) kwa kumpachika sifa ya unafiki baada ya kutoa kauli ya kwamba hoja zilizojadiliwa bungeni siku ya jana zinaashiria kuligawa taifa



    .Kilichomfanya Nassari kutumia kauli hiyo ya unafiki kwa Hussen Bashe ambapo amejumlisha pia ni sifa ya Wana CCM ni kutokana na Mbunge Bashe kupitia ukurasa wake wa Twitter kusema kwamba amepata hofu juu ya taswira ya viongozi badala ya kujadili mambo kwa msingi ya hoja na kuanza kujadili ukanda.
    "Mh. Bashe aliandika "Bungeni Leo nimeona Un holly discussion ambayo imejaa dhana ya kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukanda na Ukabila. CCM,Chadema,Cuf na NCCR tuliomo ndani ya Bunge hatuna haki yoyote ya kuanza kupandikiza mbegu ya kuligawa Taifa"
    Ameongeza "Tanu, CCM toka 1957 mpaka leo ilihimiza Umoja na Utaifa na kukemea uhalalishaji wowote wa kuligawa Taifa kwa Misingi ya Dini ukanda na ukabila" Maombi yangu kwa wananchi wenzangu msivumilie mwanasiasa yoyote yule ikiwa ni pamoja na mimi atakayekuja na hoja yenye lengo la kuwagawanya" Bashe.
    Ujumbe wa Bashe
    Baada ya mfululizo wa hoja hizo kwenye ukurasa wa Bashe , Nassari leo amejibu hoja hizo kwa kumwambia Mbunge huyo kwamba baada ya yeye kushindwa kumkemea Mwenyekiti wake kwa kutoa kauli zinazotafsiriwa kuwa ni za kibaguzi ndipo anaibuka na kusema taifa linagawanywa.
    "Unafiki ni moja wapo ya sifa kubwa ya mwanaCCM,  HusseinBashe ulishindwa kumkemea mwenyekiti wako wa chama akitoa kauli za kibaguzi kanda ya ziwa juu ya bomoa bomoa, leo wanaibuka wabunge kukemea ndio unajitokeza na kusema tunaligawa taifa?!" Nassari.
    Ameongeza kwamba "Kunyamazia uovu huu kwa kujifanya hatuuoni sio kulisaidia taifa, ni vyema na ni wakati sahihi kukemea kabla halijamea".

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI