• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 9 November 2017

    RC AYOUB ACHARUKA KASKAZINI UNGUJA KWA KUWAONDOA ASKARI WAWILI

    Askari wawili wa jeshi la polisi wanaofanya kazi za doria za utalii wameondolewa mara moja katika kitengo hicho cha doria kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa.

    Kaimu Mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja ambae pia ni mkuu wa mkoa mjini magharibi Mh. Ayoub Mahmoud alichukua hatua hiyo na kuuagiza uongozi wa jeshi la polisi mkoa huo kufuatiwa na malalamiko kutoka kwa wananchi katika muendelezo wa ziara zake za kuonana ana kwa ana na wananchi, ambapo malalamiko hayo yalitolewa na baadhi ya wananchi katika maeneo ya viwanja vya Nungwi.

    Askari hao wamelalamikiwa kufuatia kuchukua rushwa kutoka kwa watembeza wageni wasio rasmi katika ukanda wa fukwe za nungwi na kusababisha kero kwa wawekezaji na watalii wa maeneo hayo.

    Mhe Ayoub amesema agizo hilo litekelezwe mara moja huku hatua za uchunguzi kwa askari hao zikiendelea ili kupunguza masikitiko kwa wananchi juu ya tuhuma mbali mbali zinazotolewa kwa watendaji wa serikali!.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI