• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 2 November 2017

    MCT kuwapeleka mahakamani watakao wanyanyasa waandishi

    Hayo yamezungumzwa Leo na katibu mtendaji wa baraza hilo Bw.Kajubi Mukajanga Leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuongezeka kwa matukio na madhila wayapatayo wanahabari kuongezeka wakiwa kazini ambapo amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita jumla ya magazeti matano yamefungiwa likiwemo gazeti LA mseto,mwanahalisi,nawio,Tanzania daima pamoja na raia mwema pia mbali na vyombo hivo kufungiwa waandishi mbali mbali wamepata misukosuko wakati wakiwa kazini baadhi yao ni pamoja na Halfani Liundi wa ITV Arusha,ambaye aliwekwa kizuizini na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru The.

    Alexander pastory mnyeti ambaye hivi sasa amepandishwa cheo na kuwa mkuu w mkoa wa manyara mbali na hill mwandishi Augusta Njonji wa nipashe hivi karibuni aliandika habari za kamati ya bunge na hesabu  za serikali(PAC) na kukamatwa kisha kuhojiwa na Polish na baadae kuachiwa kwa dhamana,na waandishi mbalimbali  wa kutoka Mwananchi,Azam TV,na mtanzania daima huko geita nao walipata misukosuko wakati wakiwa kazini kuripoti wanafunzi wa sekondari ya Geita hivi karibuni.

    Hata hivyo Bw.Mukajanga amesema kutokana na matukio hayo na mengine mengi yanayoendelea kutokea hofu kwa waandishi wa habari na tasnia nzima wamekuwa wanashindwa kufanya kazi zao kwa Uhuru na kwa weledi kwakuhofia kufanyiwa madhila.

    Vile vile Bw.Mukajanga ameainisha sababu zinazopelekea  kufungia vyombo vya habari kwa kiasi ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka,upandishwaji wa sheria,unyanyasaji na ujahili na hata matamshi ya vitisho kutoka kwa viongizi dhidi ya wanahabari.

    Pia Be.mukajanga amemaliza kwa kuwataka wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari kuziweka Sera zao wazi ili kupunguza matatizo na madhila kwa waandishi wao.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI