• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 2 November 2017

    ,Taasisi ya Tanzania Health Summit imeandaa kongamano

    Kutokana na juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini,Taasisi ya Tanzania Health Summit imeandaa kongamano la nne la kitaifa la afya, ili kuweza kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kufikia suluhisho.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Rais wa Kongamano hilo Dkt Omary Chillo amesema kuwa kongamano hilo litafanyika tarehe 14-15 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere ,huku takribani wadau wa afya 500 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo.

    Pia amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "ni jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha upatikanaji wa afya Bora kwa kuunganisha tafiti za kisayansi ,ubunifu na sera za afya".

    "Ningependa kutoa wito kwa wadau wa afya kutoka serikalini na mashirika binafsi, mahospitali, asasi zisizo za kiserikali,taasisi za kitaaluma na wadau wengine wa maendeleo ya afya waweze kushiriki kikamilifu katika mkutano wa mwaka huu",alisema.

    Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rebecca John amewataka watanzania na wadau wote kujiandikisha kwa wingi ili kushiriki kwa pamoja kuunga juhudi za Serikali za kutatua changamoto za afya hapa nchini.

    Ifahamike kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano hilo atarajiwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya Prof Muhammed Kambi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI