Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Idukilo kata ya Idukilo alipokwenda kuhamasisha shughuli za
maendeleo.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu, Sostenes Mbwilo akifafanua jambo kuhusu umuhimu
wa wananchi kushiriki shughuli za maendeleo wakati wa mkutano huo wa
hadhara.
Diwani wa kata ya Idukilo, Sara Michael akitoa neno kwa wananchi wake katika mkutano huo.
Ofisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mang’era Mang’era (kushoto) akifafanua jambo katika mkutano huo wa hadhara.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha
Idukilo wakifuatilia mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuhamasishana
kushiriki shughuli za maendeleo katika kijiji chao.
……………………………………………………………..
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ametembelea kijiji cha Idukilo na
kuzungumza na wananchi kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katika ziara hiyo Magoiga
aliambatana na timu ya watalaamu wakiwemo Afisa Elimu Msingi, Sostenes
Mbwilo, Afisa Mipango, Mang’era Mang’era na Afisa Elimu Ufundi, Moshi
Balele.
Aliwahimiza wananchi kijijini
hapo kwenye kata ya Idukilo kushirikiana kwa pamoja katika kusimama
miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia fedha zinazotolewa.
Mkurugenzi huyo alisema wananchi
wana wajibu wa kuchangia shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule
ikiwemo vyumba vya madarasa na nyumba za walimu kwa njia mbalimbali.
“Kamati ya shule, serikali ya
kijiji na watalaamu kutoka wilayani wote mnapaswa kushirikiana kwa
pamoja katika kusimamia shughuli za miradi zinazotekelezwa katika kijiji
chenu,” alisema.
Katika mkutano huo wa hadhara pia
mkurugenzi ikiwa ni mojawapo wa utaratibu aliojiwekea, alitumia nafasi
hiyo kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi kijijini hapo.
No comments:
Post a Comment