Hayo yamezungumzwa Leo na naibu waziri Dkt.Faustine
Ndugulile katika hafla ya uzinduzi wa cheti cha mfumo wa uhakiki ubora
wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO Leo katika ofisi za mamlaka
hiyo ambapo amesema kuwa kazi zinazofanywa na TFDA zinamgusa kila MTU
kwani katika maisha ya kila siku hakuna asiyetumia bidhaa
zinazodhibitiwa na TFDA hivyo mamlaka hiyo inahakikishia umma kuwa afya
zetu zinanalindwa na kwa kufanya hivo kunakuwa na wananchi wenye afya
njema ambao wanaweza kufanya kazi na kuliletea taifa maendeleo hususani
katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Aidha mh.Ndugulile amesema mafanikio hayo ya TFDA katika
kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa chakula,dawa,vipodozi,vifaa
tiba na vitendanishi ni utekelezaji kwa vitendo wa azma ya serikali ya
awamu ya tano chini ya uongozi wa mhe.John Pombe Magufuli katika
kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya hususan upatikanaji wa
dawa,vifaa tiba na vitendanishi.
Nae Bw.HIITI B SILLO ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TFDA
ameanza kwa kumshukuru mhe naibu waziri Dkt.Ndugulile kwakufika katika
hafla hiyo pia akaeleza kuwa kuna kurugenzi NNE zilizo chini ya
mkurugenzi mkuu ambazo ni kurugenzi ya uendelezaji huduma,kurugenzi ya
usalama wa chakula,kurugenzi ya dawa na bidhaa nyongeza ns kurugenzi ya
huduma za maabara hivyo katika kusogeza huduma za udhibiti kwa wananchi
TFDA imeanzisha ofisi saba za kanda ambazo zinahudumia mikoa yote 26 ya
Tanzania na kukabidhi baadhi ya majukumu na madaraka ya TFDA
yamekasiniwa kwa wakurugenzi watendaji wa Halmashauri kupitia kanuni za
kukasimu madaraja na majukumu ya TFDA.
Vile vile Bw.SILLO ameeleza kuwa kutokana na utendaji kazi
wa TFDA wamepata mafanikio mengi katika kuweka na kusimamia mifumo ya
menejimenti na ile ya udhibiti wa ubora wa usalama wa bidhaa kwa mujibu
wa miongozo ya kimataifa ya WHO,FAO,codex na ISO.hivyo imekuwa kitovu
cha mafunzo kwa mamlaka nyingi za udhibiti barani Afrika ambapo
takribani taasisi za nchi 15 zimekuja kujifunza TFDA. Ameendelea kwa
kusema kuwa kwa kuwa mamlaka ya chakula na dawa imekuwa ikitekeleza
mfumo wa uhakiki ubora wa huduma (Quality Management System)kuanzia
mwaka 2005 baada ya kufanya tathimini ya namna bora ya kufanya shughuli
za udhibiti kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wateja hivo mfumo huo
uliimarishwa na hatimaye kufikia mwaka 2009 tulitunukiwa cheti cha
kiwangi cha kimataifa cha ubora cha ISO9001:2008.pamoja na faida
nyingine nyingi ,baadhi ya faida zilizotokana na kutekeleza mfumo huo ni
pamoja na kufanikisha kuwa na mifumo bora ya utendaji Nazi
inayozingatia matarajio na matakwa ya wateja kwenye huduma
zetu,kuboresha mawasiliano ya ndani pamoja na ya nje na kutengenezwa kwa
mipango mikakati yenye tija na inayotekelezeka.hivyo tangu tulipopata
cheti hiko kwa Mara ya kwanza tumekuwa tukifanyiwa kaguzi za kila mwaka
ili kubaini kama mfumo wetu wa uhakiki ubora wa huduma bado unakidhi
matakwa ya kiwango hicho cha kimataifa hivyo matokeo yake Yameweza
kuonyesha kuwa mfumo wetu wa utoaji huduma unazidi kuimarika siku hadi
Siku na tuliweza kuongeza wigo kwa kutekeleza mfumo huo kwenye kurugenzi
zote za TFDA na ofisi za kanda ambazo Nazo zilijumuishwa kwenye vyeti
vya kuhuisha tulivyotunukiwa mwaka 2012 na 2015.hivyo mfumo huu wa sasa
unatekelezws katika kurugenzi katiks kurugenzi na ofisi zote za kanda
za TFDA na unajumuisha shughuli za kutengeneza kufanya marejeo na
kusimamia matumizi ya nyaraka ,kufanys kaguzi za ndani za kutumia timu
ya wakaguzi,kusimamia ukaguzi wa nje wa mfumo kwa ajili ya kupewa cheti
cha usajili cha ISO,kuratibu marejeo ya mfumo yanayofanywa na
menejimenti na mwisho kutekeleza na kusimamia mfumo wa kusimamis
vihatarishi pia mfumo umetoa mwongozo katika kutengeneza mpango mkakati
wa miaka mitano wa mamlaka ambapo malengo mkakati yaliyoainishwa
yanatekelezwa na yanafanyiwa ufatiliaji kwa mujibu wa mwongozo wa ubora
uliowekwa kama nyenzo muhimu ya mfumo huu hivyo TFDA inafarijika kwakuwa
mfumo huu umekuwa ni chachu ya maendeleo makubwa yaliyofanikiwa hivyp
bado wanadhamilia kuendelea kuboreshs mfumo huu kwa kutenga rasilimali
za kutosha ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kutoa huduma Bora za
udhibiti kwa kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wetu bila kuathiri
ubora,usalama,na ufanisi wa bidhaa tunazidhibiti.
No comments:
Post a Comment