• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 30 November 2017

    RC MAKONDA AJITOLEA KUMSAIDIA AHMED ALBAITY

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA amejitolea kumsaidia Kijana AHMED ALBAITY anaesumbuliwa na tatizo la Uti wa Mgongo  lililompelekea kulala kitandani kwa takribani miaka 10.

    AHMED ALBAITY anatakiwa kwenda kutibiwa Nchini China kwa muda wa Wiki tatu akiambatana na Wasaidizi Wawili ambapo Gharama za Matibabu zinazohitajika ni zaidi ya Dola 40,000 za Marekani ambapo Sindano moja aliyoandikiwa inagharimu kiasi cha Dolla 27,000.

    RC MAKONDA  amesema atafanya jitihada zote kuhakikisha AHMED anapatiwa Matibiwa ili aweze kupona na kutimiza ndoto zake akiwa na Afya Njema.

    Mapema leo RC MAKONDA ametembelewa Ofisini kwake na Balozi Mpya wa China Nchini Tanzania Bi. WANG KE ambae amekuja kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa ambapo katika Mazungumzo RC MAKONDA  amemgusia Balozi huyo Suala la Matibabu ya  AHMED ALBAITY  ambapo Balozi WANG KE. alieambatana pia na Daktari Bingwa wa China aliebaki Nchini kwaajili ya Shughuli ya Serikali ya China ambapo wamemtazama na kupitia Ripoti ambapo wameahidi kulifanyia kazi suala hilo.

    Katika Mazungumzo hayo pia wamejadili Masuala mbalimbali ikiwemo Kuimarisha Usalama,  Kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu na kuongeza huduma kwa Wananchi.

    MAKONDA pia ameishukuru Serikali ya China kwa kuleta Meli ya Jeshi la China yenye Hospital ndali ambayo imesaidia kutoa  vipimo na Matibabu kwa wananchi wengi.

    Kwa Upande wake  .Bolozi Mpya wa China Nchini Tanzania WANG KE amesema Serikali ya China itaendelea kusaidiana na Tanzania katika  masuala yote ya maendeleo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI