• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 30 November 2017

    Wadau wa viwanda nchini waombwa kushiliki vyema kwenye onesho la pill la viwanda

    .

    Na florah Raphael.

    Ikiwa ni mwendelezo wa harakati za Tanzania kufikia uchumi wa kati kwa kutumia uchumi wa viwanda, Tan trade ikishirikiana na kamati ya maandalizi ya kitaifa ya maonyesho inayosimamiwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri mkuu, wizara ya Viwanda, biashara na uwekezaji pamoja na taasisi ya umoja wa mataifa ya maendeleo ya viwanda (UNIDO) imeandaa onesho la pili la viwanda litakalofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 11mwezi huu katika viwanja vya sabasaba.

    Akiongea Leo waziri mwenye dhamana Mh.Charles J.P Mwijage amesema kuwa maonyesho hayo ni ya pili Sasa huku yakibeba kauli mbiu ileile ya mwaka Jana inayosema "Tanzania Sasa tunajenga viwanda" ikilenga kuwahamasisha wananchi juu ya falsafa na dhima ya ujenzi wa viwanda wa uchumi wa viwanda.


    Pia mwijage amesema kuwa dhamira kubwa ya onesho hilo ni kujenga jukwaa kwa wadau wa sekta ya viwanda ili kupata fursa ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza shughuli na bidhaa zao.

    "Dhamira kubwa kuelekea onesho hilo ni kuwakutanisha wadau wote wa viwanda ili kuweza kupata fursa ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu" amesema.

    Aidha mwijage ameongeza kuwa maonyesho hayo yanalenga kuwakutanisha wadau wote wa viwanda wakiwemo wazalishaji wa malighafi, taasisi zinazotoa huduma kwa wenye viwanda pamoja na taasisi zinazosaidia kusambaza bidhaa kutoka kiwandani mpaka kufika kwa mtumiaji.

    Mwisho waziri mwijage amewahasa wote wenye viwanda kujitokeza kwa wingi kwenye onesho hilo ili kuweza kuonyesha shughuli wanazozifanya kwenye viwanda vyao, kutangaza bidhaa zao lakini pia kujifunza kutoka kwa wadau wengine watakao kutana nao kwenye onesho hilo.

    "Wote wenye viwanda kuanzia vidogo mpaka vikubwa wajitokeze kwa wingi siku hiyo ili kuonyesha kazi wanazozifanya na kutangaza bidhaa zao" amesema Mwijage

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI