Thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka shilingi bilioni
20 ya wiki iliyoisha ya tarehe 27 OCT 2017 hadi shilingi bilioni 3 kwa
wiki iliyoisha november3
Hayo yamesemwa na afisa muhandamizi wa soko la hisa Marry
kinabo alipokuwa akitoa Tathimini ya mauzo ya hisa kwa wiki iliyoisha
ambapo amesema idadi ya hisa ziliuzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa
mil 1.6 ya wiki iliyoishia OCT 27 hadi hisa mil 3.5 ya wiki iliyoisha
novemba 3 pia amezitaja kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni
TCC ambao wanaongoza kwa 41%,TBL 27%,CRDB 16%,voda 11%.
Vile vile bi.Kinabo ameendelea kwakusema kuwa ukubwa wa
mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa
shilingi bilioni 217 kutoka shilingi Trilioni 20.5 kwa wiki iliyopita
hadi shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyoisha tarehe 3 novemba2017 Punguzo
hilo limetokana na kupungua kwa bei za hisa za KA (8%), JHL(8%),CRDB(6%)
na TBL(5%).
Pia Bi.Kinabo ameendelea kwa kusema kuwa ukubwa wa mtaji wa
kampuni za ndani umepungua kwa shilingi bilioni 112 kutoka Trilioni
10.163 hadi kufika shilingi Trilioni 10.051 wiki hii na hiyo
inasababishwa kwa kupungua kwa bei ya hisa za CRDB(6%)na TBL(5%).
Kwa upande wa mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoisha
tarehe 3 Novemba yalikuwa shilingi bilioni 15.7 kutoka shilingi milioni
500 wiki iliyopita ya mwezi octoba 27,mauzo haya yalitokana na
hatifungani kumi na moja(11) za serikali na pia za makampuni binafsi
zenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 17.4 kwa jumla ya gharama ya
shilingi bilioni 15.7
No comments:
Post a Comment