Mkutano
wa tume ya haki za binadamu wa kufanya tathimini kuhusu mapendekezo ya
haki za binadamu yanayopendekezwa na umoja wa mataifa umefanyika Leo,
huku lengo kuu likiwa ni kuweka mikakati na misingi ya kujadili masuala
ya haki za binadamu na kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa sambamba
na kukuzwa.
Akizungumza
katika mkutano huo, mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu Bahame T.
Nyanduga amesema kuwa jumuiya ya umoja wa mataifa wa haki za binadamu
imeweka utaratibu wa kutathimini nchi takribani 196 ili kugundua ni
jinsi gani zinalinda na kukuza haki za binadamu kwa kuzingatia tamko la
haki za binadamu kimataifa hivyo katika tathimini ya awali Tanzania
ilipewa mapendekezo 237 na kati ya hayo serikali ilichagua mapendekezo
130 wanayoweza kuyafanyia kazi.
Pia
Nyanduga amesema kuwa bado kuna changamoto mbalimbali kwa nchi
zinazopewa mapendekezo na umoja wa mataifa wa haki za binadamu kwa
kushindwa kuyatimiza kwa wakati sahihi.
Nyanduga
ameongelea kuhusu suala na haki ya kufanya mikutano ya hadhara na
kusema kuwa haki ya kukusanyika imetamkwa kwenye katiba na ni haki ya
kila mtanzania kukusanyika na kufanya jambo lolote ambalo haliendi
kinyume na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwisho amewahasa na kuwaomba wa Tanzania wenyewe kulinda haki zao kwa kufuata misingi ya katiba kama inavyosema.
"Watanzania
wanatakiwa kulinda haki zao wenyewe kwa kutumia katiba pamoja na
mahakama ya nchi vizuri ili kupata haki zao za msingi" amesema Nyanduga
No comments:
Post a Comment