Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisistiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha wadau wa masuala ya Ajira na
Ukuzaji Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma Novemba 7, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Bw. Erick Shitindi akisisitiza jambo kuhusu mkakati wa Serikali
kuboresha mazingira ya Ajira hapa nchini walipokutana leo Mjini Dodoma katika
kikao cha Wadau wa masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw .Geodfrey Simbeye akisisitiza
jambo wakati wa Kikao cha pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha kujadili masuala ya Ajira na
Ukuzaji Ujuzi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Wenye Ulemavu Mhe. Stella
Ikupa akichangia mada kuhusu ushiriki wa watu wenye ulemavu katika programu
zinazotekelezwa na Serikali katika masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi ili
kujikwamua kiuchumi.
Wajumbe wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa kikao cha Kujadili Masuala ya Ajira na Ukuzaji
Ujuzi kilichofanyika Mjini Dodoma.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara na Huduma Bi Jane Gonsalves
akichangia hoja kuhusu mikakati ya Serikali kuwawezesha Vijana kupata ajira na
kujiajiri wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi leo
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe.
Antony Mavunde akichangia hoja kuhusu namna bora ya kuwawezesha vijana
kujikwamua kiuchumi wakati wa kikao cha Kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Novembna 7, 2017 Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Dkt.Aggrey Mlimuka
akichangia hoja wakati wa kikao cha kujadili masuala ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI
YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
No comments:
Post a Comment