VIJANA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametoa tamko la kumpongeza Rais Dk. John
Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji katika utekelezaji wa ilani
ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya Urais.
Tamko
hilo limetolewa katika kambi ya Vijana iliyokuwa ya siku tatu
ilijumuisha vijana 500 kutoka Vyuo na Vyuo vya Vikuu nchini na Vijana
kutoka Matawi katika Kata zote mkoani Mwanza ikiwa na lengo la kujenga
vijana kuwa na uzalendo, maadili bora, uongozi na kuijua vyema itikadi
ya Chama Cha Mapinduzi lengo likiwa kuwafanya pia watambue walikotoka
walipo na wanakotaka kwenda.
Kambi hiyo ya Vijana iliandaliwa na kuratibiwa na Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu kupitia Seneti ya Vyuo katika mkoa huo.
Akitoa
mada, mtoa mada mkuu kwenye kambi hiyo, Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi Humphrey Polepole aliwataka Vijana kuwa wazalendo katika taifa
lao na kuwataka wasitumike katika kukiharibu chama bali wawe walinzi na
wasimamizi wa kukitetea chama na kukosoa watendaji wabovu wanaoiangusha
serikali.
Polepole
alisema, alisema, vijana wakijengeka katika misingi bora na kuijua vema
itikadi ya CCM ndiyo wataweza kuwa na uzalendo, maadili mazuri na kisha
kuwa viongozi bora.
Akisoma
maazimio ya kambi hiyo, Katibu wa Vijana mkoa wa Mwanza Mariam Amir
alisema, Vijana waliokuwa kwenye kambi hiyo wameazimia kwa pamoja
kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa mafanikio makubwa ya kiutendaji wa
ilani ya CCM katika kipindi cha miaka yake mwili ya urais na kuahindi
kuendelea kumuunga mkono ili kuhakikisha anafanikisha zaidi kusimamia
utekelezaji wa ilani ya CCM.
Alisema,
wameazimia hivyo kwa sababu Rais Dk. Magufuli katika kipindi hiki cha
miaka miwili ameweza kusimamia mambo muhimu ya kuendeleza nchi ikiwemo
katika sekta ya elimu, ujenzi wa reli standard geuge, ununuzi wa ndege,
ujenzi barabara, bomba la mafuta, makusanyo ya kodi, udhibiti wa upotevu
rasimali za umma na nidhamu ya watumishi wa umma.
Mariam
alisema Vijana pia wameazimia kuitumikia CCM kwa moyo na nguvu zao zote
na kuahidi kuwashughulikia wote wanaokwenda kinyume na maelekezo ya
Chama na kutokubali kutumikia mtu zaidi ya kutumikia chama na kuahidi
kupeleka ngazi za chini elimu na maarifa ya mafunzo waliyoyapata kutoka
kambi hiyo kwa wanachama hasa vijana katika ngazi ya matawi na mashina
ili kuendelea kuimarisha itikadi ya chama.
Alipokaribishwa
kuzungumza kwa nafasi yake ya Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu,
iliyoandaa kambi hiyo, Daniel Zenda aliwakumbusha vijana wajibu wa kila
mwanachama katika kukisemea chama na serikali yake katika mafanikio
yaliyotekelezwa kupitia ilani ya CCM
Zenda
aliwataka pia vijana nchini kote kupambana kwa vitendo na wale wote
wanaojaribu kubeza na kupotosha ukweli kuhusiana na jitihada
zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli
katika utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Alisema
umefika wakati sasa wezi na wanaotumia rasilimali za nchi kwa manufaa
yao sasa kujondoa weneyewe ndani ya Chama kwa kuwa CCM Mpya imeimarisha
misingi yake chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli na sasa
siyo kichaka cha kujifichia wezi.
“Bila
shaka mmeshuhudia baadhi wakianza kuondoka wenyewe ndani ya CCM, sasa
subirini watazidi kuondoka wezi wengi ndani ya CCM maana kwa sasa hawana
namana ya kufanaya zaidi ya kukimbia”, alisema Zenda.
No comments:
Post a Comment