Katibu Mkuu wa Madini, Profesa
Simon Msanjila akizungumza na watumishi wa Idara ya Madini iliyo chini
ya Wizara ya Madini (hawapo pichani) kwenye kikao kilichofanyika jijini
Dar es Salaam mapema leo Novemba 06, 2017
Sehemu ya watumishi kutoka Idara
ya Madini iliyo chini ya Wizara ya Madini wakisikiliza maelekezo kutoka
kwa Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani)
Sehemu ya watumishi kutoka Idara
ya Madini iliyo chini ya Wizara ya Madini wakisikiliza maelekezo kutoka
kwa Katibu Mkuu wa Madini, Profesa Simon Msanjila (hayupo pichani)
…………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Madini, Profesa
Simon Msanjila leo tarehe 06 Novemba, 2017 katika Ofisi za Wizara ya
Madini zilizopo jijini Dar es Salaam amekutana na watumishi wa Idara ya
Madini lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mikakati ya namna ya
kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika
ukuaji wa uchumi wa nchi. Profesa Msanjila aliwataka watumishi kufanya
kazi yenye matokeo chanya kwa ubunifu wa hali ya juu ili sekta hiyo
ichangie zaidi katika uchumi wa nchi. Pia amewataka watumishi kuendana
na hali ya mabadiliko yaliyotokea katika sekta hiyo. Katika hatua
nyingine, Katibu Mkuu amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuwasilisha
taarifa za utendaji kazi pamoja na changamoto zake. Wakati huohuo,
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka alimkaribisha
Katibu Mkuu na kuahidi kutoa ushirikiano ili kuboresha utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment