Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
amedai uchumi wa Tanzania ni mzuri na unakua kwa kasi ndio maana miradi
mikubwa imeanzishwa na inatekelezwa katika kipindi hiki pamoja na
kuaminiwa kukopa na Benki kuu ya Dunia.
Rais Magufuli amesema kuwa uchumi mzuri sio lazima mtu awe na pesa
nyingi chumbani bali ni pamoja na kuwa na ugumu katika utafutaji hela.
SOMA NA HII- Rais Magufuli awatumbua Wakurugenzi wawili Bukoba
“Ninapowaeleza kuwa uchumi wetu ni mzuri, ni mzuri kweli kuwa
na uchumi mzuri hauna maana kuwa na mahela umeyajaza chumbani. Uchumi
ni pamoja na kuwa na hela ngumu kuipata, kizuri hakipatikani hovyo
hovyo, ni lazima utoe jasho. Nilikuwa nazungumza juzi pale Mwanza kuwa
bajeti ya Afya imepanda kutoka bilioni 31 hadi bilioni 269 na Tanzania
tukapewa nafasi ya kuuza madawa katika nchi zote za SADC.“amesema
Rais Magufuli leo tarehe 6 Novemba 2017 mkoani Kagera wakati wa
ufunguzi wa mradi wa wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani
Kagera
..
Monday, 6 November 2017
Habari
No comments:
Post a Comment