Raia hao ambao wengi wao wanatoka
maeneo ya Fizi na misisi Kivu kusini mwa Congo wamedai kuwa Vikosi na
wapiganaji wa maimai nchi Congo na vikundi mbalimbali vya waasi
vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu na hivyo kuanza kukimbia
nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Wakizungumza mbele ya kamati ya
ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyotembelea katika kituo cha
kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia hao walisema sababu
iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa maisha yao
kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na Serikali
iliyopo madarakani.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia
Jenerali (mst.) Emannuel Maganga akiongoza kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika kuwaona raia hao na wanafana
jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma muimu za kibinadamu
zinaboresha katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya kusikiliza maombi
ya ukimbizi inajiadaa kuwasikiiza raia hao.
Kutokakana na wimbi kubwa hilo
huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi zinahitajika haraka ili
kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na watoto.

Baadhi ya raia waliokimbilia
nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na kuahirishwa Uchaguzi Mkuu
uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka kwa mzozo wa mapigano
uenda ukawaathiri amani nchini Congowa, Vyama vya upinzanu vimeanza
kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi, wamehofia amani.
Kituo cha kigadye wilayani kasulu,
huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia wa Congo wanaoendelea
kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini mwao. Kusini mwa
Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio ya mara kwa mara
yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment