• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 4 December 2017

    Africa yadhamiria kukabiliana na sumu kivu

    Na Stahmil Mohamed
    Kutokana na kuongezeka kwa tatizo la sumu kuvu kwenye vyakula hasa kwenye zao la mahindi ambalo takribani nchi 16 kutoka Afrika zinategemea zao hilo, umoja wa afrika kupitia programu ya udhibiti wa aflatoksini barani afrika (PACA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine imeadaa kongamano kwa lengo la kupunguza ongezeko la aflatoksini katika vyakula.
    Akiongea Leo Raymond Wigenge ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya usalama wa chakula TFDI amesema kuwa aflatoksini inasababisha madhara makubwa katika usalama wa chakula na pia huadhiri afya za watu na maendeleo yao.
    Pia Raymond amesema kuwa inakadiliwa kuwa watu milioni 208 katika bara la afrika wanategemea mahindi kama chakula chao kikuu ambapo nchi 16 kati ya 22 ulimwenguni ambazo zinategemea mahindi kama chakula chao kukuu, ziko barani afrika.
    "Nchi 16 kati ya 22 ulimwenguni zinazotegemea zao la mahindi kama chakula kikuu zinatoka barani afrika" amesema Raymond.
    Pia ameongeza kuwa kongamano hilo linawaunganisha kwa pamoja watalaam kutoka vyama vya wakulima, wataalam wa kilimo, watalaam wa afya, watalaam wa lishe pamoja na wafanya biashara ili kwa pamoja waweze kugundua njia bora ya udhibiti wa usambaaji wa sumu kuvu kwenye mahindi barani afrika.
    "Katika kongamano hili tutakuwa na vyama mbalimbali kama vile vyama vya wakulima, watalaam wa afya, watalaam wa kilimo, watalaam wa lishe pamoja na wafanya biashara ili kwa pamoja waweze kugundua njia bora ya udhibiti wa usambaaji wa sumu kuvu kwenye mahindi barani afrika".
    Pia Raymond amebainisha hasara na madhara yanayotokana na sumu kuvu kuwa ni kansa ya maini, kudumaa kwa watoto, lakini pia amesema kuwa bara la afrika hupoteza milioni 600 za kimarekani kwa mwaka kwa kutupa mahindi yaliyochafuliwa na sumu kuvu.
    "Afrika hupoteza milioni 600 za kimarekani kwa kutupa mahindi yaliyochafuliwa na sumu kuvu lakini pia sumu kuvu husababisha Kansa ya maini na kudumaa kwa watoto" amebainisha Raymond.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI