Habari
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita leo ameondoka jijini hapa kuelekea Chicago Nchini Marekani kuhudhuria
mkutano wa Mameya kutoka sehemu mbalimbali duniani utakaofanyika Desemba 4 hadi
7 mwaka huu.
Mkutano huo unatarajiwa kuhusisha Mameya 182 kutoka
sehemu mbalimbali Dunia ambapo pamoja na mambo mengine watajadili suala la utawala
bora pamoja na utumishi wa viongozi kwa wananchi.
Aidha katika mkutano huo pia wataangalia na
kujadili changamoto za majiji makubwa hususani katika sekta ya Afya,
miundombinu, Maji safi na salama, Elimu pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Desemba 5 Mameya wote waliohudhuria mkutano huo kwa pamoja
watashindanisha majiji yaliyofanya vizuri katika sekta ya miundombinu ambapo
jiji la Dar es Salaam limeingia kwenye ushindani huo kupitia mradi wa mabasi yaendayo haraka.
Aidha katika ushindani huo, Meya Mwita
amesema kuwa ana amini kwamba jiji la Dar es Salaam litaibuka mshindi wa tuzo
hiyo kwa kuwa mradi huo umekuwa ukifanya vizuri katika sekta ya usafirishaji na kwamba watanzania wajiandae
kwa ajili ya kupokea tuzo hiyo.
Majiji mengine ambayo yanameingia kwenye
ushindani huo mbali na jiji la Dar es Salaam ni Mji wa Cape Town, Cairo pamoja
na majiji mengine Dunia. Meya Mwita atarajea Nchini Desemba 8 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment