Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mbeya kimepata pigo
baada ya kumpoteza moja ya mwanachama wao na kiongozi, Jacob Kalua
ambaye amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

"Kamanda Jacob Kalua, ni pigo lingine kwa Mbeya na Kanda ya Nyanda za juu (Nyasa) kwa jumla. Tutaukosa ujasiri wako, hasa kipindi hiki cha siasa za kibabe na mabavu, kipindi ambacho makamanda wasio waoga kama wewe wanahitajika zaidi kwenye kazi ya ukombozi" alisema Joseph Mbilinyi
Mbali na Sugu pia Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche ameonyesha kusikitishwa na kifo cha kiongozi huyo na kusema kuwa alikuwa msaada mkubwa katika chama
"CHADEMA imepoteza mpiganaji asiechoka nakumbuka nikiwa Mwenyekiti wa BAVICHA mara zote nilizokuja Mbeya ulivyonipokea, nakumbuka maandalizi yako ya mikutano, ulinzi na hata kuhakikisha tumekula vizuri. Tangulia mbele ya haki kaka ila umetuachia maumivu makubwa"
No comments:
Post a Comment