• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 13 December 2017

    Watanzania watakiwa kujiandaa kifikra wakati wowote ,kuepukana na mawazo yaliyopitiliza ili kuepukana na matatizo ya afya ya Akili pamoja na maradhi ya moyo

    Na Stahmil Mohamed
    .
    Hayo yamesemwa na Daktari wa chuo kikuu cha sayansi na tiba muhimbili professa Karim Manji alipokuwa akizungumza katika warsha ya fikrafya iliyofanyika Leo lengo likiwa ni kutoa mafunzo kuhusiana na matatizo ya afya ya Akili na jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo ambapo amesema kuna haja ya kujitaarisha kifkra ili kuepukana na maradhi ya moyo yanayotokana na mawazo yakupiliza pamoja na matatizo ya Akili na kuwataka watanzania wachukulie changamoto mbalimbali wanazozipata ni za mda na zipo hivyo wasikate tamaa na kujikataa moja kwa moja kwakujiona hawafai katika jamii jambo ambalo sio la kweli na ni hatari kwa afya ya Akili pamoja na mwili.

    Professa Manji ameendelea kwa kueleza kuwa japo si rahisi binadamu kukosa mawazo ila amewataka wasipitilize kufikiria kwakuwa athari zake ni kubwa kwa afya ya akili na moyo na ndio maana wameamua kukutana kujadili na kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wakiwemo walimu,wanasheria,manesi pamoja na madaktari ili kupata matokeo chanya kwenye jamii ili kukabiliana na tatizo hili

    Naye Mwenyekiti wa Fikrafya Dkt Shabil Hussein amesema wameamua kuielimisha jamii kuhusiana na matatizo ya ubongo na Akili kwenye jamii kwa kuwa ni tatizo ambalo jamii wanalichukulia kwa mtazamo tofauti kuwa kila mwenye tatizo la akili ni lazima awe na muonekano ambao haufanani na watu wengine Bali kuna aina nyingi ya magonjwa ya Akili kwani kunabaadhi ya watu wapo maofisini wanakabiliwa na matatizo ya Akili yanayotokana na mawazo yaliyopitiliza(stress)kutokana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kila siku hivo wanajipanga kutoa elimu nchi nzima kuhusiana na matatizo ya afya ya Akili na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazosababisha

    Pia Daktari bingwa wa afya ya akili Dkt Saidi Kuganda amesema kupitia warsha ya Leo ya mafunzo maalumu ya kwa wadau mbalimbali ameona jamii itafaidika kupitia mafunzo hayo pia jamii itaelimika kuhusiana na afya ya elimu ameendelea kwa kusema kuwa takwimu inayotolewa kuwa kila watu 4 mmoja anawezekana akawa na matatizo ya afya ya akili hiyo haimaanishi kuwa ni wameathirika zaidi hivyo elimu itakayotolewa kuhusiana na   afya ya akili kupitia fikrafya itakuwa chachu ya kuelimika katika jamii.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI