Na Stahmil Mohammed
Baraza la Taifa la ujenzi limekutana na wadau wa sekta ya ujenzi kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zilizopo katika sekta ya ujenzi kwa lengo la kuimarika na kuendelea kuzidi kujenga uchumi wa nchi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inajikita katika uchumi wa Viwanda.
Baraza la Taifa la ujenzi limekutana na wadau wa sekta ya ujenzi kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zilizopo katika sekta ya ujenzi kwa lengo la kuimarika na kuendelea kuzidi kujenga uchumi wa nchi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inajikita katika uchumi wa Viwanda.
Hayo yamesemwa na mtendaji mkuu wa baraza la Taifa la
ujenzi Mhandisi Matiko Samson Mturi ambapo amesema katika mkutano huu
umewahusisha
wakandarasi,watengenezaji wa vifaa vya ujenzi ,wasambazaji
wa vifaa, watu wa Bima,Wizara ya ujenzi, vyama vya kutetea
wakandarasi,ewura,wabunifu majengo na wadau mbalimbali wa ujenzi wakiwa
na lengo moja la kuwasikiliza wote hao changamoto wanazokabiliana Nazo
ili wazipatie ufumbuzi kuboresha zaidi sekta ya ujenzi kuleta tija
katika nchi.
Akizianisha baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowabili ni
pamoja na ukosefu wa uzoefu wa ujenzi wa miradi mikubwa kama wa reli wa
standard Gauge unahitaji uzoefu mkubwa hivyo kupitia changamoto hiyo
wataangalia namna gani serikali itawasaidia katika kuwawezesha kupata
ujuzi zaidi kupitia wahandisi wakigeni wanaokuja kutekeleza miradi hiyo
wanawapatia mafunzo.
Naye mkurugenzi wa Sera na mipango Wizara ya ujenzi
uchukuzi na mawasiliano mhandisi Elizabeth Taghora amesema katika
mkutano wa Leo kutapatikana ufumbuzi wa kila changamoto zilizopo katika
sekta ya ujenzi na kuhakikisha sekta ya ujenzi inaimarishika na inazidi
kuchangia uchumi wa nchi kwa kuwa sekta ya ujenzi ni miongoni mwa sekta
zinazotegemewa nchini hasa katika harakati za Sasa za kuelekea uchumi wa
viwanda na ndio maana wadau wote wa sekta ya ujenzi wamekutana kujadili
changamoto mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi wenye tija.
Vile vile katibu wa chama cha makandatasi wa barabara
Magret Ngianaeli amesema wamesema kupitia mkutano wa leo wa majadiliano
watahakikisha wanatoka na Sera ambayo itawapa usawa makandarasi wazawa
na kipaumbele zaidi ili wazidi kusikika na kupata fursa zaidi za kazi na
uzoefu.
No comments:
Post a Comment