Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana leo
ameteuliwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais John Pombe
Magufuli kuendelea kuwa katika nafasi yake kwa kipindi kingine.

''Namshukuru ndugu Kinana kwa msaada wake mkubwa alionipa kwa kipindi chote hicho nafikiri anafaa kuendelea kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi kingine,'' amesema Magufuli. Kauli ya Rais Magufuli inaondoa tetesi zote zilizokuwa zinadai kuwa Kinana ameandika barua ya kuomba kujiudhuru katika nafasi yake kwa kilichodaiwa kuwa haridhishwi na utendaji wa Mwenyekiti wake Rais Magufuli.

Kinana aliwahi kuwa mtumishi wa Jeshi la Tanzania kwa miaka 20 pamoja na kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki mwaka 2001 hadi 2006, amechaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu 2012.
No comments:
Post a Comment