
Shamsa Ford ameendelea kutia mkazo kuwa Irene Uwoya ndiye msanii mzuri kuliko wasanii wanawake wote na kusema labda kidogo ambaye anamkaribia Ray C na kudai Irene Uwoya amejaaliwa karibu kila kitu kuhusu muonekano na kusema yeye muda mwingine huwa anadhani lile ni jini.

Aliendelea kusema kuwa "Mbaya zaidi ni mzuri na ana mvuto akipita lazima akusitue. Maana kuna wengine wazuri lakini hawana mvuto wakipita kama hajapita mtu..Wanawake kusifiana ni ngumu ila mimi niko tofauti huwa siwezi kuacha kumsifia mtu pale anapofanya jambo zuri au ana vitu ambavyo huwezi acha kumsifia. Narudia tena Iren ni mwanamke mzuri mwenye mvuto kuliko wanawake wote wa bongo movie hadi wanamziki amewafunika. Ingekuwa enzi zile angeshindana na dada yangu Ray c maana ndo mwanamziki wa kike ninaeonaga ana mvuto na mzuri" alisema Shamsa Ford
No comments:
Post a Comment