• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 19 December 2017

    Nilipata kazi kumtetea - Kikwete

    Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ya Tanzania na mwenyekiti mstaafu wa CCM, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ameelezea ugumu alioupata wakati wa mchakato wa kumpata mrithi wake kuiongoza CCM, ambapo aliyependekezwa alikuwa ni Rais John Magufuli.
    Akizungumza na wana-CCM waliohudhuria mkutano mkuu ambao ulifanya uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wa chama hiko Taifa, Jakaya Kikwete amesema alipata ugumu kumtetea Magufuli kwa sababu kwenye wasifu wake hakuwa kushika wadhifa wowote ndani ya chama hiko, na kuhofia huenda akashindwa kuongoza.
    "Tulipokuwa kwenye mchakato, moja ya kazi kubwa nilikuwa nayo kama mwenyekiti ni kutetea kwamba Magufuli anafaa, na hoja mojawapo ni kwamba hajawahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi, hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa shina, atawezaje kuwa mwenyekiti, anatoka tu paaap kuwa mwenyekiti wa taifa", amesema Jakaya Kikwete.
    Hapo jana Rais Magufuli amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kupata kura zote halali 1821.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI