Mbunge
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Dk. Godwin Oloyce Mollel ametangaza kujivua rasmi
uanachama wa chama hicho na kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.
Mollel
ametangaza kujiuzulu ubunge wake kwa madai ya kwamba sasa anafurahishwa
na uongozi wa Rais Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi ya
Tanzania, hivyo yeye hana sababu ya kuendelea kupingana tena na chama
cha CCM
Pia ameongeza kuwa anaungana na CCM katika kuleta maendeleo maana ameona
dhamira ya kweli ya Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.
Soma zaidi barua yake
No comments:
Post a Comment