• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 14 December 2017

    MWANASHERIA WA GGM MBARONI KWA KUMNYIMA NYARAKA NAIBU WAZIRI

     
    Mwanasheria
    Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo akipandishwa kwenye gari ya Polisi Baada ya agizo la  
    Naibu
    Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola.
     
    Mwanasheria Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) David Nzarigo
    amekamatwa na serikali baada ya kukutwa na nyaraka za serikali .
                                                                                                                                       
    Mwanasheria huyo amekamatwa kwa  amri ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
    Muungano na Mazingira Mh,Kangi Lugola alipotembelea Mgodi huo ambapo pamoja na
    mambo mengine amebaini mgodi huo kuwa unaendesha shughuli zake bila kufuata
    sheria ya mazingira .
    Mhe. Lugola akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili  Wilayani Geita ameagiza kukamatwa kwa
    mwanasheria  Mkuu  wa Mgodi wa dhahabu wa  Geita (GGM) David Nzogila baada ya kukutwa na
    nyaraka za serikali ambazo hazijawa rasmi kutumika kutoka taasisi  ya wakala wa utafiti wa jiolojia
    Tanzania(GST).
     Hata hivyo katika hali hisiyo ya kawaida na  bila kutarajia mwanasheria huyo aliyekuwa akiukingia kifua mgodi huo  ili usikumbane na rungu la fidia ya uharibifu wa kimazingira kama sheria
    inavyotamka alijikuta akimweleza Naibu Waziri kuwa anayo ripoti ya GST aliyodai
    haijaeleza iwapo mgodi huo unahusika moja kwa moja kwenye uharibifu hivyo mgodi
    huo usibebeshwe mzigo huo.
    Kutokana na hali hiyo,Naibu Waziri Lugola aliomba apatiwe riporti hiyo ili ajiridhishe lakini mwanasheria huyo akijibu kwa kujiamnini alimtaka kiongozi huyo wa juu   kutumia mbinu zake kuipata Serikalini lakini yeye  hawezi kutoa nyaraka ya serikali, jambo  lililomkasirisha Naibu Waziri  wa Muungano na Mazingira na kutoa agizo la kukamatwa mara moja.
     
    Diwani wa kata ya mtakuja Constatine Morandi ameelezea kuwa wananchi wamekuwa wakisumbuliwa muda mrefu na mgodi bila ya kupatiwa fidia  na kwamba kutokana na wao kuwa ndani ya bikoni kumesababisha kutokupatiwa huduma mbali mbali za kijamii  hivyo ni vyema kwa serikali wakaweka nguvu kuwasaidia wananchi hao.
     
    Bw Abdallah Omary-Mkazi Nyamalembo alimweleza Naibu waziri  kwamba wamekuwa wakiishi
    maisha ya mashaka kutokana na hali ilivyo ya maeneo hayo ya mgodini na kwamba
    mgodi ulikwisha wai kuwapatia fidia ya shilingi elfu ishirini jambo ambalo
    limeonekana kuwa ni udhalilishaji kwani pesa hiyo ni ndogo.
     Kwa upande wake Makamu wa Rais wa mgodi huo Saimon Shayo,alisema kuwa  eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu suala la fidia hadi sasa kuna nyumba mbili na kwamba fidia ya kwanza
    walilipa kiasi cha sh,Bilion Moja na waliipatia serikali iweze kuwafidia
    wananchi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI