• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 8 December 2017

    SHIRIKA LA UMEME TANESCO LASHINDA TUZO YA UFANYAJI KAZI MZURI KWENYE SEKTA YA FEDHA



    Shirika la Umeme TANESCO latunukiwa tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu katika mwaka wa Fedha wa 2016/2017 na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania(NBAA)katika Ukumbi wa APC Hotel,tuzo hiyo ilipokelewa na Afisa Mkuu wa Fedha kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Bi.Renata Ndege .

    Afisa Mkuu wa Fedha kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Bi.Renata Ndege alisema anaishukuru bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania(NBAA)  nchini kwa kutambua utendaji  kazi wa TANESCO na kutoa hati safi na wanatarajia mwakani watachukua ushindi wa jumla.

    Pia ameiahidi bodi hiyo kuwa watazidi kuimarisha utendaji wao wa kazi kwenye swala zima la hesebu katika shirika hili.

    Aidha amesema shirika kwa kushirikiana na Bodi  litakikisha linafuata utaratibu unaopangwa na bodi hiyo.


    Tuzo hiyo inaonyesha utendaji kazi Wa shirika hilo usio wa mashaka , jamii iendelee kuliamini shirika hilo kwani wapo kwaajili ya kuwahudumia wananchi.

    pia anasema  tuzo hiyo inaonyesha namna wanavyofanya kazi katika viwango vya kimataifa


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI