• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 27 December 2017

    Usipojipendekeza kwa Mkuu inakula kwako - Mrisho

    Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka Wakuu wa shule mbalimmbali mkoani humo kuhakikisha fursa zinagawanywa kwa usawa kwa walimu wote na kutaka dhana ya walimu wanaojipendekeza tu kwa mkuu wa shule kuwa wanufaika wa fursa hizo inakufa.
    Mrisho Gambo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na baadhi ya walimu wa shule ya  Embarway Sekondari iliyopo Arusha na kusema kama walimu Wakuu wakifanya utaratibu mzuri itasaidia walimu hao kunufaika na fursa mbalimbali kwa usawa, jambo ambalo litasaidia kuondoa upendeleo.
    "Kumekuwepo na malalamiko sehemu zingine kwenye zoezi kama la leo hili la kusimamia mitihani unakuta kila mwaka wanakwenda walimu wale wale rafiki zake Mkuu wa shule, kama wewe kiwango chako cha kujipendekeza ni kidogo wewe utakuwa unasikia kwa wengine tu maana orodha ya walimu wanaokwenda kwenye usimamizi huwa inapagwa na Mkuu wa Shule, maeneo mengine nasikia wanaangalia sana jinsi kama ni mdada akimpa ushirikiano zaidi Mkuu wa Shule huyo dada hakosi lakini tumekuwa tukisisitiza hiyo kazi ya kusimamia mitihani ni kazi ya kila mwalimu" alisema Gambo
    Aliendelea kufafanua kuwa "Kwa Mkuu wa shule anayejitambua anapaswa kutengeneza utaratibu mzuri ili kuwe na mzunguko, kila mwalimu mwenye sifa aweze kushiriki kwenye zoezi hilo, haiwezekani ukaenda kila mwaka, unaweza kwenda mwaka huu mwakani akaenda mwingine, baadaye ikafika tena zamu yako. Kwa sababu walimu hawa hawana kazi ya ziada, ofisi zingine wanalipwa masaa ya ziada lakini walimu hawalipwi, mwalimu hana posho, mwalimu hana safari, mwalimu yeye ni mitihani, sensa na kusimamia uchaguzi basi sasa hizo fursa zinapaswa kuwekewa utaratibu mzuri ili kila mmoja anufaike nazo" 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI