• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday 24 December 2017

    Wazazi waombwa kuwaacha watoto wafanye wanachokipenda



    Na Stahmili Mohammed.

    Wazazi wametakiwa kuachana na mila na desturi za kizamani na kuwapa watoto wao ushirikiano sambamba na kuwatia moyo ili wasikate tamaa  kwa kile wanachopenda kufanya.

    Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es salaam katika mapokezi ya mshindi wa  miss world university Afrika yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julias Nyerere na Ester John ambaye ni mama mzazi wa Queen Elizabeth Makure aliyeshinda tuzo ya miss world university.

    Ester amesema kuwa watoto kugombea umiss siyo kwamba wanajihusisha na mambo yasiyofaa Bali ni kipaji kama vilivyo vipaji vingine.

    "Mtoto kugombea umiss siyo kwamba ni uhuni Bali ni vipaji kama vilivyo vipaji vingine" amesema Ester john.

    Hata hivyo kwa upande wake Queen Elizabeth ambaye ndiye mshindi wa miss world university, amesema kuwa anafuraha kubwa sana kushinda nafasi hiyo kwani anaamini kuwa Sasa amekuwa balozi wa nchi yake na kuahidi kuwa ataiwakilisha nchi hasa katika suala la kutetea amani.

    "Nafurahi sana kushinda tuzo hii na ni imani yangu kuwa Sasa nimekuwa balozi wa nchi yangu na nitaiwakilisha nchi hasa katika suala la kutetea amani" amesema Queen Elizabeth.

    Pamoja na hayo Queen Elizabeth amewahasa vijana wenzake walioko vyuoni na majumbani wasikubali kukatishwa tamaa na mtu yeyote kwani ukiwa na bidii hakuna jambo lisilowezekana.

    "Vijana wenzangu walioko vyuoni na mtaani wasikubali kuyumbishwa wala kukatishwa tamaa na yeyote, ukitia bidii hakuna lisilo wezekana"amesema Queen Elizabeth.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI