Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, imemhukumu mkazi wa mtaa
wa barabara ya Mbutu, Mohamed Ahmed (54) kifungo cha miaka mitatu jela
baada ya kutiwa hatiani kwa kumtishia na kumtolea lugha ya matusi Mkuu
wa Wiilaya hiyo, John Mwaipopo.

Mwendesha
Mashtaka wa Serikali, Elimajidi Kweyamba, alidai mahakamani hapo kwamba
mshitakiwa, alitenda kosa hilo Januari 09, mwaka huu, saa 1:05 usiku
katika maeneo ya barabara kuu ya lami ya Igunga mjini.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Igunga, Ajali Milanzi, Kweyamba amesema kuwa mshitakiwa huyo alimtolea Lugha ya matusi Kiongozi huyo wa Wilaya wakati akitekeleza majukumu ya agizo la upandaji miti kama lilivyotolewa maelekezo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani.
Aidha, mwendesha mashtaka amedai kwamba katika kosa la pili, muda huo huo na tarehe hiyo hiyo, mshitakiwa akiwa na nia ovu, alimtishia maisha kwa maneno Mkuu wa Wilaya kuwa atamwonyesha na atahakikisha anahama Igunga kwa kumfanyia kitu kibaya.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka yote mawili, mshtakiwa huyo alikiri kutenda makosa hayo.
Kabla ya kutoa hukumu, Hakimu Milanzi alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mwenyewe makosa, atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu gerezani, mwaka mmoja kwa kosa la kwanza na miwili kwa kosa la pili.

No comments:
Post a Comment