• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 January 2018

    Arsenal yavunja rekodi yake

    Klabu ya soka ya Arsenal hatimaye imevunja rekodi yake ya usajili baada ya kutumia kiasi cha £ 56 milioni (Bilioni 156) kukamilisha usajili wa nyota wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund.
    Arsenal imekamilisha usajili huo mchan huu ikiwa ni siku chache tu tangu imuuze nyota wake raia wa Chile Alexis Sanchez kwenda Manchester United.

    Taarfia ya Arsenal imeeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa muda mrefu wa kuitumikia klabu hiyo yenye masikani yake Emirates. Muda mchache ujao wanatarajia kuweka wazi mkataba huo.

    Aubameyang ambaye sasa ndiye mchezaji ghali zaidi ndani ya Arsenal ameifungia Dortmund mabao 141 katika mechi 213 alizoichezea kwenye mashindano yote.

    Msimu wa 2017/18  Aubameyang amefunga mabao 13 katika mechi 16 za ligi kuu ya soka Ujerumani  Bundesliga. Mchezaji bora huyo wa Afrika mwaka 2015 ameivunja rekodi ya Mesut Ozil aliyesajiliwa kwa £42.5 millioni (Bilioni 119).

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI