• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 January 2018

    Watanzania waombwa kumuombea Mzee Majuto

    Mke wa Mzee Majuto ambaye anafahamika kwa jina la Aisha Mbwana amefunguka na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombe Mzee Majuto ili aweze kupona maradhi ambayo yanamsumbua na kusema sasa hivi mumewe amelazwa katika hospitali ya Tumaini. 
    Akiongea na moja ya chombo cha habari nchini Aisha amesema kuwa toka jana majira ya saa kumi jioni alipokwenda kwenye hospitali hiyo ya Tumaini walilazwa kutokana na mume wake kusumbuliwa na tatizo la tezi dume ambalo limeanza kumsumbua takribani miezi miwili sasa.

    "Tumekuja hospitali kuanzia jana saa kumi jioni na tumelazwa kwani Mzee Majuto anaumwa anasumbuliwa na tatizo la tezi japo kuwa hayupo 'serious' sana kama ambavyo watu wanafikiria, napenda kuwaambia Watanzania na mashabiki wa Mzee wazidi kumuombea Mungu kwa sababu bado tunamuhitaji", amisema Aisha Mbwana

    Kwa upande wake Mzee Majuto akiwa hospitali hapo ambapo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji aliweza kuongea na kusema kuwa yeye anazidi kupambana kuhakikisha anatibu ugonjwa huo na kudai kuwa kuugua ni ibada.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI