• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 January 2018

    Ozil naye akubaliana na Arsenal

    Winga wa Ujerumani Mesut Ozil amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu kuendelea kubaki Arsenal mpaka mwezi Juni 2021.
    Mkataba huo mpya unamfanya Ozil sasa kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ndani ya klabu hiyo kiasi cha £ 350,000 (Bilioni 979) kwa wiki kabla ya kukatwa kodi.

    Leo ni siku nzuri kwa Arsenal ikiwa imetoka kukamilisha usajili wa Pierre Aubameyang kutoka Borrusia Dortmund. Mkataba wa awali wa ozil ulikuwa unamalizika mwezi juni mwishoni wa msimu huu.

    Ozil mwenye miaka 29 alijiunga na washika mitutu hao wa jiji la London mwaka 2013 akitokea klabu ya Real Madrid kwa dau la rekodi ya klabu £ 42.4m (Bilioni 119) ambayo leo imevunjwa na usajili wa Aubameyang kwa dau la £ 56 (Bilioni 156).

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI